Kero la usalama nchini Misri

Mmoja wa waandamanaji akiwa amelal chini baada ya kujeruhiwa huko Giza.
Miongoni mwa majeruhi waliojeruhiwa jana

Watu 18 wameuawa tangu kutokea milipuko mjini Cairo siku ya Ijumaa
Vikosi vya usalama vimewekwa katika hali ya tahadhari wakati ambapo mikutano miwili ya makundi hasimu nchini Misri ikitarajiwa kufanyika ili kuadhimisha miaka mitatau ya kuondolewa madarakati kwa rais wa zamani Hosni Mubarak.
Wafuasi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi pamoja na wale wa serikali inayoungwa mkono na jeshi wanatarajiwa kufanya maandamano katika miji mikubwa nchini humo.

Hali ya wasiwasi iliongezeka hapo jana baada ya misururu ya milipuko ya mabomu na ghasia katika maeneo tofauti nchini humo ambayo imesababisha vifo vya watu 18 huku wengine wakijeruhiwa.

Vuguvugu la Muslim Brotherhood limeshutumu milipuko hiyo lakini wapinzani wake wamelikosoa kundi kwa kuendeleza mashambulizi kama hayo.

Inaarifia wapiganaji wamezidisha mashambulizi dhidi ya utawala wa Misri, huku milipuko kadhaa ikisikika katika mji mkuu Cairo

Mashambulizi hayo yanatokea katika mkesha wa kuadhimisha mwaka wa tatu tangu kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa Rais Hosni Mubarak.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company