Wajumbe wa mazungumzo ya usitishwaji wa mapigano ya Sudan Kusini wakiwa Addis-Abeba, walifanikisha utilianaji saini huko Ethiopie, le 23 janvier 2014.
REUTERS/Birahnu Sebsibe
Na RFI
Umoja wa mataifa UN umearifu kuwa Majeshi ya Serikali ya Sudani kusini na upinzani yaliendelea na mapigano licha ya Viongozi wa utawala wa Sudan Kusini na wale wa upande wa waasi, kutiliana saini ya kusitisha mapigano usitishwaji ambao ulitekelezwa mnamo saa kumi na moja na nusu kwa saa za Sudan Kusini.
Kwa mujibu wa naibu msemaji wa umoja wa mataifa UN huko Sudan Kusini Farhan Haq amebainisha kuwa ni kweli baada ya kusainiwa kwa usitishwaji wa mapigano katika baadhi ya maeneo kulishuhudiwa mapigano ambayo yalitulia baadaye.
Waasi wanaomuunga mkono Rieck Machar wamewatuhumu majeshi ya Sudani Kusini kuwashambulia muda mfupi kuelekea kusitishwa kwa mapigano hayo ambako kulifikiwa huko Adis Ababa Ethiopia,madai ambayo majeshi ya serikali yamekana kujihusisha na mashambulizi yoyote tangu baada ya kusainiwa kwa mkataba wa kusitisha mapigano.
Ni uamuzi uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na jumuiya ya kimataifa ambayo mara zote imekuwa ikizishinikiza pande hizo mbili kufikia makubaliano ya awali ambayo kwanza yalitaka kusitishwa kwa mapigano nchini humo ili kutoa nafasi ya mazungumzo zaidi ya amani kupata muafaka.