Mashambulizi yamekuwa yakiongezeka mjini Mombasa.
Mkuu wa polisi mjini Diani, Jack Ekakuro, amesema washambuliaji hao waliilenga baa moja iitwayo
Tandoor mjini Diani mapema leo, wakati ilipokuwa bado imefurika watu waliokuwa wakiendelea kusherehekea mwaka mpya. Hii ni sehemu ya mlolongo wa mashambulizi, ikiwa ni pamoja na lile la bomu kwenye basi moja katika mtaa wa Eastleigh mjini Nairobi mwezi uliopita, hali inayowatia wasiwasi Wakenya wengi.
Mwandishi: Diana Kago
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
