KWA mwaka wa pili mfululizo, Uturuki imeshika namba moja kwa kuwafunga jela waandishi wa habari, ikifuatiwa kwa karibu na nchi za Iran na China. Kwa pamoja nchi hizo tatu zinachangia zaidi ya nusu ya kesi zote za waandishi wa habari waliofungwa jela duniani kote, Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ) imebainisha.
“Kuwafunga waandishi wa habari kutokana na kazi zao ni ishara ya ukosefu wa uvumilivu, jamii iliyo kanzamizi,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa CPJ, Joel Simon.
“Inaumiza kuona idadi ya waandishi waliofungwa ikiongezeka katika nchi kama Vietnam na Misri. Lakini kusema kweli inashtusha kuona Uturuki ikiongoza kwa kuwafunga jela waandishi wa habari kwa mwaka wa pili mfululizo.” Alisema.
CPJ ni taasisi huru isiyolenga faida inayofanya kazi kwa ajili ya kulinda na kutetea uhuru wa habari duniani.
Mbali ya vinara watatu wa ufungaji jela wanahabari duniani, wengine wanaoingia kati 10 bora ni Eritrea, Vietnam, Syria, Azerbaijan, Ethiopia, Misri na Uzbekistan.
Kwa jumla kulikuwa na waandishi 211 katika kuta za magereza hadi kufikia Desemba mosi, mwaka jana. Hata hivyo, CPJ haijaorodhesha waandishi wengi waliofungwa na kuachiwa kipindi cha mwaka huo.
Idadi ya waandishi waliofungwa na utawala wa Rais Bashar al-Assad ilipungua hadi 12 kutoka 15 wa mwaka 2012, lakini pia takwimu hizo hazihusishi makumi ya waandishi waliotekwa na wanaoaminika kushikiliwa na makundi yenye silaha ya upinzani.
Kufikia mwishoni mwa 2013, waandishi takribani 30 walikuwa hawajulikani waliko nchini Syria. Kuna mabadiliko yanayoonekana dhahiri ya idadi ya wafungwa magerezani mwaka jana.
Vietnam ilikuwa ikishikilia waandishi 18 wakiwa wameongezeka kutoka 14 mwaka 2012, baada ya mamlaka kuwaandama hadi wanablogu.
Nchi mpya zilizoingia katika takwimu hizo mwaka jana kuilinganisha na mwaka juzi ni Jordan, Urusi, Bangladesh, Kuwait, Macedonia, Pakistan, Jamhuri ya Kongo, Marekani na Misri ambayo ilikuwa ikishikilia waandishi watano.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago