Mawaziri wa Iran na Uturuki kujadili mgogoro wa Syria


Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wa Uturuki wanatarajiwa kujadili uhusiano wa pande mbili na hali inavyojiri nchini Syria ili kujaribu kuutafutia suluhisho la amani mgogoro huo. Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anatarajiwa kuwasili leo nchini Uturuki kwa mwaliko wa waziri mwenzake wa nchi hiyo Ahmet Davutoglu ambapo pamoja na mambo mengine mazungumzo yao yataangazia mgogoro wa Syria.
Hayo yanajiri huku mapigano yakiripotiwa kati ya makundi ya waasi ya Syria yanayopigana dhidi ya serikali ya Damascus katika miji ya Aleppo na Idlib. Mapigano hayo yamejiri kati ya kundi liitwalo jeshi la mujahidina, linalojumusiha makundi 8 ya wanamgambo wa Syria dhidi ya kundi linaloitwa serikali ya Kiislamu Iraq na Sham. Makundi hayo yanayoungwa mkono na nchi za Magharibi yametangaza vita baina yao na kuelekezeana kidole cha tuhuma mbalimbali, hali inayoonesha kusambaratika nguvu za waasi hao.
www.hakileo.blogspot.com
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company