Riek Machar, makamu wa zamani wa rais wa Sudan Kusini ameionya serikali ya Juba isithubutu kuwanyonga wafungwa wa kisiasa wanaoshikiliwa na utawala huo wa hasimu yake Rais Salva Kiir Mayardit. Machar ameyasema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Asharq Al Awsat linalochapishwa mjini London, Uingereza sambamba na kukosoa kile alichokisema kuwa ni Rais Kiir kutotekeleza ahadi zake za kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa ambao ni wanachama wa Harakati ya Wananchi na kuongeza kuwa, Rais Kiir anapanga njama ya kuweka mahakama ya kimaonyesho kwa lengo la kuwanyonga wafungwa hao. Hivi sasa Machar anaongoza uasi dhidi ya serikali ya Rais Salva Kiir, kufuatia kufutwa kazi na rais huyo mwezi Julai mwaka uliopita. Kwa upande mwingine kiongozi huyo wa waasi ameituhumu serikali ya Uganda kuwa inaingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo changa barani Afrika na kusema kuwa, Rais Yoweri Museveni amekuwa akizishawishi nchi wanachama wa jumuiya ya kieneo ya mashariki mwa Afrika (IGAD) kuingilia mgogoro wa Sudan Kusini katika hali ambayo nchi hizo haziko tayari kuchukua hatua hiyo. Hii ni katika hali ambayo Mkuu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Sudan Kusini ametoa wito wa kusitishwa haraka mapigano nchini humo ili kutoa fursa kwa mazungumzo ya amani yaliyokuwa yanatarajiwa kuanza leo huko Addis Ababa, Ethiopia.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago