Kamanda wa operesheni ya kutokomeza kundi la waasi la ADF-Nalu, mashariki mwa DRC, Mamadou Ndala Mustafa (katikati)
Na RFI
Mkuu wa operesheni ya kijeshi iliyokua imepangwa kutokomeza kundi la waasi kutoka Uganda ADF-Nalu, masharikia mwa Jamuhuri ia Kidemokrasia ya Congo, ameuwawa katika shambulizi la kuvizia linalosadikiwa kuendeshwa na waasi wa kundi la ADF-Nalu, na kusababisha majonzi na masikitiko kwa wanajeshi wake.
"Nina habari za kusikitisha . Kanali Mamadou N'Dala ameuwawa. (...) Inavyoonekana, ni waasi wa kundi la ADF- Nalu ambao wamemuua pamoja na wa walinzi wake wawili . Kwa kweli jeshi na taifa la Congo limempoteza shujaa”, msemaji wa serikali Lambert Mende amekiambia kituo cha habari cha AFP.
Mende amesema kwamba Mamadou N'Dala alikuwa njiani akijielekeza katika eneo la Eringeti , kilomita 54 na mji wa Beni akipeleka kikosi cha wanajeshi wakati gari lake lilishambuliwa kwa kombora lililorushwa kutoka upande wa pili wa barabara.
Shambulizi limefanyika katika kijiji cha Matembo, mjini Beni, katika mkoa tajiri wa kivu ya kaskazini la Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi.
M'moja kati ya walinzi wake alienusurika katika shambulizi hilo, amesema, wamefyatuliwa kombora kutoka upande wa pili wa barabara na kuteketeza gari aliyokuwemo.
Mlinzi huyo amesema kwamba alijitahidi kufyatua risase hovyo ili kuwatawanya waasi hao bila mafaanikio.
Mwandishi wa habari wa AFP, ambaye alitembelea eneo la tukio, amesema ameona mwili wa Kanali Ndala ukiwaka moto, huku wanajeshi wakilia kutokana na kifo cha mkuu wao.
Kabla ya kutangazwa kwa kifo cha Kanali Ndala , AFP mwandishi wa habari wa AFP, amesema, ameona wanajeshi watano wa jeshi la Congo, ambao wamejeruhiwa , wakipelekwa hospitalini katika mji wa Beni, umbali wa kilomita kumi kusini mwa kijiji cha Matembo.
Kundi la waasi la ADF- Nalu liliundwa katika miaka ya 1990 kutoka kwa muungano wa makundi mawili ya waasi yanayompinga rais Yoweri Kaguta Museveni, ambae yuko madarakani tangu mwaka 1986.