Marekani yalaani mauwaji ya mkuu wa zamani wa ujasusi Rwanda

Mlango mkuu wa kuingia Hoteli Michelangelo ambako mwili wa Kanali Karegeya ulipatikana huko Johannesburg Jan 2, 2014
Marekani imelaani mauwaji ya mkuu wa zamani wa ujasusi wa Rwanda Patrick Karegeya aliyepatikana ameuliwa ndani ya hoteli ya kifahari ya Johannesburg, na kueleza wasi wasi wake kutokana na matamshi ya hivi karibuni ya rais Paul Kagame dhidi ya wapinzani wake.
Karegeya aliyekua mpinzani mkali wa Kagame kwa miaka ya hivi karibuni alipatikana na alama za majeraha kwenye shingo, na polisi wa Afrika Kusini wanasema hiyo inaonesha huwenda alinyongwa.

Akizungumza na waandishi habari Alhamisi msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani Jen Psaki anasema "tunalaani mauwaji ya afisa wa zamani wa Rwanda Kanali Patrick Karegeya aliyekua akiishi uhamishoni Afrika Kusini."

Anasema Marekani inapongeza hatua ya Afrika Kusini kuanza mara moja uchunguzi wa kifo cha afisa huyo. Hata hivyo Psaki anasema, " hebu nifafanuwe hapa kwamba, tumekerwa na mfululizo wa kinachoonekana kuwa ni mauwaji yaliyochochewa ya Wanyarwanda mashuhuri wanaoishi uhamishoni. Matamshi ya hivi karibuni ya Rais Kagame, nikimnuku, wataona chamtemakuni wale wanaoisaliti Rwanda, ni ya kutia wasi wasi."

Karegeya alikua mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi ya masuala ya kigeni aliyewahi kuwa mshirika mkuu wa Rais.Kagame.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company