Seleka wadhibiti mji ulioko kaskazini mwa Bangui

Wanamgambo wa Muungano wa Seleka wameudhibiti mji ulioko kaskazini mwa Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Taarifa zinasema kuwa, wanamgambo hao wameudhibiti mji wa Bouca baada ya wanamgambo wa Kikristo wa kundi la Anti Balaka kuukimbia mji huo na kuelekea katika mji wa Bossangoa moja kati ya ngome kuu za kundi hilo la Kikristo. Taarifa zimeongeza kuwa, wanamgambo wa Seleka wanataka kuelekea upande wa magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa lengo la kukomboa maeneo ya mpakani kati ya nchi hiyo na Cameroon. Mapigano makali nchini humo yalianza mwezi Machi 2013 baada ya wanamgambo wa Sekela kuiangusha serikali ya Rais Francois Bozize na kushadidi zaidi mwezi Disemba mwaka huohuo yalipoanza mashambulizi mapya ya wanamgambo wa Anti Balaka. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Aprili liliafiki mpango wa kuwepo wanajeshi elfu kumi na moja na mia nane nchini humo kufikia katikati ya Disemba mwaka huu.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company