Algeria yapongezwa kuteua mawaziri 7 wanawake


Umoja wa Mataifa umeipongeza serikali ya Algeria kwa kuteua wanawake saba kushika nyadhifa za uwaziri na kuielezea hatua hiyo kuwa ni ya "kihistoria" na "mfano wa kuigwa" na nchi jirani za Kiarabu. Mkurugenzi wa Kanda wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya nchi za Kiarabu Bi Samira El-Tewegry ametoa taarifa akibainisha furaha yake na jinsi anavyojivunia hatua hiyo ambayo haijawahi kushuhudiwa katika serikali za nchi zote za Kiarabu. Taarifa hiyo imesisitiza pia kuhusu imani ya Umoja wa Mataifa juu ya suala la usawa na uwezeshaji wanawake na kuongeza kwamba Algeria imejionyesha kuwa ni mfano wa kuigwa na nchi za Kiarabu. Mabadiliko katika baraza la mawaziri la Algeria yamefanyika baada ya Rais wa nchi hiyo Abdul aziz Bouteflika kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita na kuchaguliwa kuiongoza tena Algeria kwa kipindi cha nne licha ya kuwepo wasiwasi mkubwa juu ya afya yake. Bouteflika aidha amemteua tena Abdel-Malek Sellal kuwa Waziri Mkuu baada ya kujiuzulu mwezi Februari ili kuongoza kampeni za uchaguzi za kiongozi huyo. Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais tarehe 5 mwezi huu imeeleza kuwa Rais Abdul azizi Bouteflika ameteua baraza la mawaziri ambalo limetoa asilimia 20 ya nafasi zote kwa wanawake, kwa mashauriano na waziri wake mkuu…/
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company