Habari zinasema kuwa, kundi la kigaidi la Boko Haram limeua watu wasiopungua 125 kaskazini mashariki mwa Nigeria, baada ya kushambulia mji wa Gamboru Ngala ulioko karibu na mpaka wa nchi hiyo na Cameroon. Ahmed Zanna, seneta wa eneo hilo amesema kwamba mji huo uliachwa bila ulinzi baada ya askari wake kupelekwa maeneo ya kaskazini karibu na Ziwa Chad katika operesheni za kuwatafuta wasichana waliotekwa nyara na kundi la Boko Haram.
Hayo yanajiri huku polisi ya nchi hiyo ikitangaza zawadi ya naira milioni 50 sawa na dola 300,000 kwa yeyote atakayetoa taarifa zinatazopelekea kuokolewa wasichana zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundi hilo. Serikali ya Nigeria inafanya jitihada za kuwatafuta wasichana hao wa shule waliotekwa nyara mwezi uliopita katika eneo la Chibok na kupelekwa kusikojulikana.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago