Na Zaituni Kibwana, Dar es Salaam
MCHEZAJI na kocha wa zamani wa Simba SC, Jamhuri Mussa Kihwelo ‘Julio’ amechukua na kurudisha fomu ya kugombea Umakamu wa rais wa klabu hiyo- lakini pia akasema yeye bado ni kocha halali wa timu hiyo.
Julio amechukua fomu ya kuwania umakamu wa Rais kwenye uchaguzi wa Juni 29, mwaka huu na akasema ataushitaki uongozi unaomaliza muda wake chini ya Mwenyekiti Alhaj Ismail Aden Rage kwa kumdhulumu haki yake.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, alisema ameanaudai uongozi unaomaliza muda wake milionI 24 kama fedha za mshahara. Aliema tayari amekwenda mahakamani kuwasilisha malalamiko yake kuhusu fedha hizo.
Julio akiwa Msimbazi kurudisha fomu ya kugombea
Julio kikao kilichowatoa madarakani kilikaa chini ya makamu mwenyekiti Joseph Itang’are kilikuwa batili.
“Mimi bado ni kocha wa Simba kwa kuwa uongozi uliompindua Rage kikao chake kilikuwa sio haliali na mimi bado ni kocha halali wa timu hiyo.
Alisema Rage alirudishwa madarakani na rais wa TFF Jamal Malinzi kwa kusema kikao hakikuwa halali sasa na sisi pia ni makocha halali.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago