Rais Catherine Samba-Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amewataka Waislamu wanaoishi katika mji mkuu Bangui kutoondoka mjini humo. Rais huyo wa serikali ya mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema hayo alipokutana na wawakilishi wa taasisi zisizokuwa za serikali, na sambamba na kusisitiza udharura wa kulindwa tofauti za kikabila na kidini katika mji mkuu amewataka Waislamu kutoondoka mjini humo.
Bi. Samba-Panza pia amekiri kuwa hadi sasa mamia ya Waislamu wamekimbia mji wa Bangui kwa hofu ya machafuko na mapigino na kusema kuwa, ni lazima serikali iwalinde zaidi Waislamu wanaoishi kwenye mji huo. Kwa miezi kadhaa sasa Waislamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekuwa wakishambuliwa na genge la Wakristo la Anti Balaka, huku nyumba zao na misikiti ikibomolewa.
Hayo yanajiri huku Marekani ikimuwekea vikwazo rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize pamoja na watu wengine wanne waliohusika katika machafuko na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago