Ayatullah Jaafar Sobhani mmoja kati ya wanazuoni wakubwa nchini Iran ameukosoa vikali utawala wa Saudi Arabia kwa kuharibu turathi za Kitauhidi na Kiislamu nchini humo. Ayatullah Sobhani ameutaka utawala wa Saudi Arabia kutilia umuhimu zaidi usalama wa mahujaji wa Nyumba Tukufu ya al Kaaba wakati wa msimu wa ibada ya Hija. Ayatullah Sobhani amesema kuwa, kumuheshimu na kumkirimu mgeni zilikuwa ni sehemu ya mila na desturi za Waarabu tokea kale na kusisitiza kwamba watawala wa Saudi Arabia wanapaswa kukomesha vitendo vya kutukanwa na kuvunjiwa heshima maulamaa wa Kishia wakati wa msimu wa hija. Ayatullah Sobhani ameeleza kushangazwa kwake na matamshi ya baadhi ya maulamaa wa Indonesia ambao wanatoa fatuwa ya jihadi dhidi ya Mashia katika hali ambayo baadhi ya taasisi za Kikristo zimekuwa zikifanya mahubiri na kuwashawishi Waislamu kwa mbinu mbalimbali ili waritadi, lakini maulamaa hao wamekuwa wakifumbia macho hatari hiyo inayoukabili Uislamu na Waislamu.
CHANZO http://kiswahili.irib.ir/