STRAIKA LA UJERUMANI LAOMBA KUSAJILIWA LIGI KUU YA BARA, KAZI KWENU SIMBA NA YANGA

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
MTANZANIA anayechezea klabu ya SPBGG 1914 Selbitz ya Ujerumani, Charles Mishetto amesema anataka kurudi nyumbani kucheza kwa msimu mmoja ili kujitangaza kabla ya kurejea tena Ulaya.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kutoka Ujerumani jana, mshambuliaji huyo wa timu hiyo ya Jijini Munich amesema kwamba anataka kuja nyumbani kucheza ili aonyeshe uwezo wake aweze kuitwa timu ya taifa na baada ya hapo wakala wake atamrudisha Ulaya.

Kifaa hicho; Charles Mishetto kushoto akicheza Ujerumani, anataka kurudi nyumbani

“Najua njia pekee ya kuonekana nacheza nyumbani na watu kunijua na kuujua uwezo wangu ni kucheza timu ya taifa, na ili nicheze timu ya taifa lazima nionekane nacheza nyumbani,”alisema.
Mishetot anayechezea timu ya Daraja la Nne Ujerumani amesema kwamba anaamini akipata timu Tanzania ataitwa timu ya taifa, kwa sababu anaamini juu ya uwezo wake.
“Mtu akisikia ligi daraja la nne anaweza kudharau, lakini ni ligi moja yenye ushindani na ngumu, pengine kuliko ya huko nyumbani. Ndiyo maana nataka nije huko nicheze watu waone uwezo wangu,”alisema.
Mishetto ameomba timu itakayoonyesha nia ya kumsajili iwasiliane BIN ZUBEIRY ambayo itaunganisha mawasiliano baina yao.

CHANZO BIN ZUHEIRY


Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company