Maandamano Ethiopia:Tisa wauawa



Ramani ya Ethiopia

Wanafunzi wapatao tisa wamefariki dunia wakati wa maandamano ya siku kadha katika jimbo la Oromia nchini Nigeria.

Hata hivyo, mtu aliyeshuhudia tukio hilo ameiambia BBC kuwa watu 47 waliuawa na majeshi ya usalama.

Amesema maandamano ya Ambo, kilomita 125 magharibi mwa mji mkuu Addis Ababa yalianza Ijumaa wakipinga mipango ya kupanua mji mkuu huo hadi katika maeneo ya jimbo la Oromia.

Serikali haijasema namna vingi vya vifo hivyo vilivyotokea lakini mkaazi huyo wa Ambo anasema aliona wanajeshi wakifyatua risasi za moto.

"Niliona zaidi ya miili 20 mitaani," amesema.

"Najificha ndani ya nyumba yangu kwa sababu naogopa."

Mkaazi huyo wa Ambo amesema wanafunzi wanne waliuawa Jumatatu na wengine 43 waliuawa katika msako mkali Jumanne, baada ya maandamano makubwa yaliyohusisha pia watu wasio wanafunzi.

Tangu wakati huo, mitaa ya mji huo imekimbiwa, amesema, benki na maduka vimefungwa na hakuna usafiri.

Amesema shughuli za ufundishaji zimesitishwa katika chuo kikuu cha Ambo, ambako maandamano yalianzia, na wanafunzi walizuiwa kuondoka.

Katika taarifa yake serikali ya Ethiopia imesema watu wanane walipoteza maisha wakati wa ghasia za maandamano hayo yaliyoongozwa na "majeshi ya kupinga amani" katika miji ya Ambo na Tokeekutayu, na katika chuo kikuu cha Meda Welabu, ambacho pia kiko katika jimbo la Oromia.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company