TANZANIA KATIKA MTIHANI MGUMU LEO MBELE YA NIGERIA

Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
MBIO za kuelekea Senegal kwenye Fainali za vijana chini ya umri wa miaka 20 zinaendelea leo kwa mechi kadhaa kupigwa nchi tofauti, nchini Tanzania, wenyeji Ngorongoro Heroes wakiwakaribisha Nigeria ‘Flying Eagles’.
Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Saa 10:00 jioni, viingilio vinatarajiwa kuwa Sh. 5,000 kwa VIP na 2,000 kwa sehemu nyingine zote zilizobaki.
Flying Eagles iliyofikia hoteli ya Sapphire Court, Kariakoo na msafara wa watu 32, inayofundishwa na kocha Manu Garba ni moja ya timu tishio na maana yake Tanzania ina mtihani mgumu leo.

Kila la heri vijana; Serengeti Boys kazini leo

Ngorongoro Heroes ambayo katika raundi ya kwanza iliitoa Kenya kwa jumla ya mabao 4-3 chini ya kocha wake John Simkoko na Msaidizi wake Mohamed Ayoub, itajaribu kuwa timu ya kwanza ya vijana nchini kupata ushindi dhidi ya timu za Magharibi mwa Afrika kihistoria.
Nigeria ambayo pamoja na Afrika Kusini, Angola, Benin, Burkina Faso, Cameroon, Gabon, Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Mali, Misri, Morocco na Zambia zimeanzia moja kwa moja raundi ya pili kutokana na ratiba iliyopangwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) haijawahi kukosa Fainali za zozote za vijana Afrika.
Mechi nyingine za wikiendi hii ni kati ya Msumbiji vs Zambia, Malawi vs DRC, Sierra Leone vs Ghana
Burkina Faso vs Mali zilizotarajiwa kuchezwa jana wakati leo ni Libya vs Tunisia, Ethiopia vs Afrika Kusini, Burundi vs Cameroon, Rwanda vs Gabon, Kongo vs Benin, Togo vs Morocco, Liberia vs Ivory Coast, Sudan vs Misri na Lesotho vs Angola.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company