Eneo la ukaguzi la jeshi la Ukraine mjini Slaviansk, mei mosi mwaka 2014.
REUTERS/Baz Ratner
Na
RFISerikali ya Ukraine imezindua operesheni ya kijeshi kuwasaka na kuwaondoa waasi wanaoiunga mkono serikali ya Urusi, na ambao wanadhibiti majengo ya serikali mashariki mwa nchi hiyo. Operesheni hiyo imeanzia katika mji wa Slaviansk, ambao waasi wamekuwa wakikabiliana na maafisa wa usalama kwa wiki kadhaa sasa katika shinikizo la kuwataka waondoka katika mji huo.
Kiev inasema operesehni hiyo ilianza Ijumaa asubuhi na waasi hao wameshambulia ndege yao ya kijeshi na kusabisha kifo cha rubani wa ndege hiyo. Rais wa Ukraine Oleksandr Turchynov amesema pia kuwa jeshi lake liko tayari kupambana ikiwa wanajeshi wa Urusi wapatao 40,000 wanaopiga kambi katika mpaka wa nchi hiyo awataondolewa.
Mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani, yameendelea kuishtumu Urusi kwa kuwa na njama ya kuivamia Ukraine na pia kuvunja mkataba wa kimataifa uliofikiwa juma liliopita kuowaondoa wafuasi wake katika majengo ya serikali ya Kiev na kuondoa wanajeshi wake nchini humo.
Slaviansk: vizuizi wiliyowekwa na waasi, mei mosi mwaka 2014.REUTERS/Baz Ratner
Urusi inasema haina jeshi nchini Ukraine na pia imeishtumu mataifa hayo kwa kuendeleza machafuko hayo na pia kulaani kuiwekea vikwazo vya kiuchumi. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel leo Ijumaa anakutana na rais wa Marekani Barrack Obama jijini Washington DC kujadili mzozo huu wa Ukraine na Urusi.
Waasi wanao unga mkomno serikali ya Urusi wamethibitisha kwamba polisi ikishirikiana na jeshi wameanzisha operesheni dhidi ya ngome zao. “Maafisa wa usalama wameendesha shambulio kubwa”, amesema msemaji wa waasi, akibaini kwamba helikopta ya jeshi la Ukraine imedunguliwa.
Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani, ambayo inatambua kudunguliwa kwa helikopta hio, rubani wa ndege hio aliuawa na wanajeshi wengine walijeruhiwa kwa kombora liliyopiwa dhidi ya helikopta ya kijeshi. Wizara hio imebaini kwamba ngome kuu ya wa waasi imetokomezwa. Video hii ni ya wenzetu wa France 24 kuhusu operesheni hii ya jeshi la Ukraine.