UN: Joseph Kony anajificha Sudan Kusini

Umoja wa Mataifa umesema kuwa, kiongozi wa kundi la Kikristo la Lord’s Resistance Army (LRA), Joseph Kony na baadhi ya makamanda wake wanajificha katika maeneo yanayozozaniwa nchini Sudan Kusini. Kwenye ripoti kwa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu vitendo vya Kony na kundi lake la LRA, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesema habari za kuaminika zinaonyesha kuwa, Kony anajificha katika eneo la Kafia Kingi. Eneo hilo liko Sudan Kusini na linapakana na Sudan na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ban amesema Sudan ina habari kamili kuhusu anakojificha mkuu huyo wa LRA ingawa inajifanya haijui lolote. Serikali ya Khartoum imekuwa ikikanusha tuhuma kwamba inampa hifadhi kiongozi huyo wa waasi. Joseph Kony anakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC ya kutenda uhalifu wa kivita na jinai dhidi ya binadamu. Inadaiwa kwamba makosa hayo aliyatenda wakati wa mapigano na serikali ya Uganda.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company