Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini, Mark Lippert aliyeshambuliwa siku ya Alhamisi, Machi 5, 2015.
Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini, Mark Lippert, amejeruhiwa katika shambulio lililofanywa na mshambuliaji mwenye silaha mjini Seoul.
Vyombo vya habari vya Korea Kusini vinaeleza kwamba Lippert, mwenye miaka 42 alipelekwa katika hospitali kwa matibabu baada ya kushambuliwa Alhamisi asubuhi kwa saa za Korea Kusini.
Ripoti zinasema, balozi Lippert alikuwa anatoka damu kutoka katika jeraha usoni lakini alitembea mwenyewe wakati anapelekwa hospitali.
Taarifa zinazidi kusema Lippert, alishambuliwa katika upande wa kulia wa kidevu chake na wembe.
Akiongea na kituo cha televisheni cha CNN msemji wa wizara ya mambo ya nje Marie Harf, amesema balozi huyo alipelekwa hospitali na taarifa zilikuwa bado hazijakusanywa za sababu ya shambulizi hilo.
Rais Barack Obama alimpigia simu balozi huyo na kumpa salamu za pole, na kumuombea apone haraka.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago