Mwanamke anayedaiwa kuwa na sura mbaya duniani na mitandao inayomuonea ametoa filamu kuhusu maisha yake.
Maisha ya Lizzie Velasquez mwenye umri wa miaka 26 yalibadilika kabisa baada ya kuona kanda ya video katika mtandao wa tube iliodai kwamba yeye ndiye mwanamke mwenye sura mbaya duniani.
Lizzie ambaye alikuwa na miaka 17 wakati huo alikasirishwa kuona kwamba msichana aliyekuwa katika kanda hiyo ya video alikuwa yeye.
Kanda hiyo ilioonekana mara millioni 4 mtandaoni huku wengi wakiwacha ujumbe wa kuudhi kama vile ''angeuliwa alipozaliwa'',nilishangaa nilipoona ujumbe huo alisema Lizzie.Lizzie
Ujumbe mwengine ulisoma ''kwa nini wazazi wake walimlea''.
Mwanamke huyo alipiga moyo konde na kuanza mtandao wake wa You Tube akiwaelezea watu kuhusu mwanamke huyo anayedaiwa kuwa mwenye sura mbaya zaidi.
Lizzie amesema kuwa anawasaidia wengine ambao wamekuwa wakionewa kuweza kupata msaada ama hata kupambana na maonevu hayo.
Mwanamke huyo pia anafanya kazi na Tina Meir ambaye mwana wao Mega alijiuwa baada ya kuonewa katika mtandao.
CHANZO BBC SWAHILI