Polisi nchini Uganda iliwaokoa watoto 24 kutoka kwenye kambi inayoaminika kuwa ya mafunzo ya kijeshi ya waasi wa kundi la Allied Democratic Forces-ADF, la nchini Uganda.
Watoto hao inasemekana kuwa wana umri kati ya miaka 2 na 15, na polisi walisema wana ushahidi wa video kuthibithisha kwamba watoto wamekuwa wakipatiwa mafunzo ya vita.
Ripoti ya mwandishi wetu Kennes Bwire wa Uganda
Taarifa zaidi zinasema kwamba watoto walivalishwa mavazi ya ki-Islam ya Hijab, Taribush na Kanzu kwenye makazi yao yaliyopo Mpoma katika wilaya ya Mkono iliyopo nje kidogo ya jiji la kampala eneo la mashariki mwa Uganda.
Msemaji wa polisi nchini Uganda, Fred Enanga anasema kuna ushahidi wa picha za video zinazoonyesha watoto hao wakipatiwa mafunzo yanayoaminika kufanywa na kundi la waasi la ADF la nchini Uganda. “tulifanikiwa kuwaokoa watoto wachanga waliokuwa wakiishi maisha ya kuhuzunisha, malezi mabovu katika mazingira machafu n ahata kulishwa vibaya”.
Wakati huo huo waalimu wa watoto hao waliotambulika kwa majina ya Athuman Naluwoga na Abdurashid Mbazira walikamatwa na wanaripotiwa kuwa ni wanachama wa kundi la uasi la ADF. Mafunzo yalikuwa yakitolewa kwenye nyumba mbili zilizojengwa kwa matope zilizokuwa zikitumika kama madarasa na mabweni kwa wavulana 12 na wasichana 12.
Polisi nchini Uganda hivi sasa inawatafuta wazazi wa watoto hao.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago