Wachezaji wa Yanga wakishangilia mojawapo ya mabao yao.
Simon Msuva akiichambua ngome ya Platinum.
Amissi Tambwe akipambana na mabeki wa FC Platinum wakati wa mechi
Hatuna Niyonzima akishangilia bao la pili aliloifungia Yanga.
Mrisho Ngassa akiipangua ngome ya Platinum
Mashabiki wa Yanga roho safiiiiii... baada ya ushindi wa 5-1.
MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga,wameichabanga FC Platinum ya Zimbabwe mabao 5-1 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mchezo wa mzunguko wa kwanza wa kombe hilo kwa Yanga baada ya awali kuwatoa BDF XI ya Botswana kwa mabao 3-2.
Wafungaji wa mabao ya Yanga ni Salum Telela, Haruna Niyonzima, Amissi Tambe na Mrisho Ngassa (2) huku bao pekee la FC Platinum likiwekwa wavuni na Walter Musona.CHANZO:GLOBALPUBLISHERS