Dr Abel Kinyondo & Invited Expert Innocent Bash from TEITI addressing the media .
Expert Mr Dennis Rweyemamu (Head - Policy and Research, UONGOZI INSTITUTE) answering questions.
January Makamba and Mujobu Moyo listening to participants.
January Makamba answering questions from participants.
Moderator discussing topics with participants .
· Iwapo kutakuwepo ushirikishwaji wa wananchi
· Wataalamu nao watoa yao ya moyoni
KUTOKANA na kugundulika kwa hazina kubwa ya gesi nchini ambayo inategemewa kukuza pato la taifa zaidi ya mara 15 ya sasa, kiasi cha kuiwezesha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.
Hata hivyo, dhana ya kwamba Rais ajaye baada ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake, anaweza akaikuta Tanzania ikiwa ni nchi tajiri tayari kutokana na rasilimali hiyo ya gesi asili, inaweza isiwe sahihi kama hautawekwa mfumo madhubuti wa ushirikishwaji wa wananchi katika fursa zilizopo katika rasilimali hiyo, sera, sheria na usimamiaji mzuri wa raslimali hiyo.
Pia itawezekana tu iwapo viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali hiyo watahakikisha wanaisimamia kikamilifu kwa mujibu wa sera na sheria zitakazotungwa na kusimamiwa na viongozi wenye dhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania na nchi yao kwanza.
Hayo pamoja na mengine yalijadiliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Watanzania wapatao 400 kutoka wilaya mbalimbali ambapo walitoa maoni yao kuhusu ni jinsi gani mapato yatakayotokana na gesi yatawanufaisha wananchi wote wa Tanzania.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago