Ugiriki yashindwa kulipa deni la IMF

Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Christine Lagarde(kushoto) akiwa na waziri wa fedha wa Ugiriki, Yanis Varoufakis

Ugiriki imeshindwa kutekeleza muda uliowekwa kulipa deni la Shirika la Fedha Duniani, IMF la euro bilioni 1.6, saa chache baada ya mawaziri wa umoja wa nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro kukataa kuongeza muda wa kulipa deni hilo ili kunusuru uchumi wa Ugiriki.

Lakini mawaziri hao wamesema watajadili pendekezo la Ugiriki katika mpango mpya wa kunusuru uchumi.

Ugiriki ni nchi ya kwanza iliyoendelea kushindwa mkopo wa IMF katika muda uliopangwa na sasa ni rasmi inakabiliwa na malimbikizo ya deni hilo.

Kuna wasiwasi kwamba hali hii itaiweka Ugiriki katika hatari ya kuondoka katika umoja wa nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro.

IMF imethibitisha kwamba Ugiriki imeshindwa kulipa deni lake muda mfupi baada ya kumalizika kwa muda uliokuwa umepangwa jana, Jumanne.

"Tumeiarifu Bodi ya Wakurugenzi kwamba Ugiriki kwa sasa iko katika malimbikizo ya deni na itaweza kupata fedha kutoka IMF, mara itakapolipa malimbikizo, amesema msemaji wa IMF Gerry Rice.

Kwa kumalizika kwa muda wa kulipa deni la umoja wa nchi za euro, Ugiriki haitapata mabilioni ya fedha za euro na imeshindwa kutekeleza muda uliopangwa kulipa deni la IMF.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company