Baada ya Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kutangaza kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chadema jana katika ukumbi wa Bahari Beachi jijini Dar es salaam, chama cha Mapinduzi kimetoa taarifa ya kuzungumza na Vyombo vya Habari leo.
Taarifa hiyo ya chama cha Mapinduzi haijafafanua kuwa ajenda itakuwa nini katika kikao hicho lakini kwa mujibu wa watafiti wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa kikao hicho kitakuwa maalumu kwa ajili ya kujibu shutuma zilizotolewa na Lowassa kuhusiana na madai ya kuwepo uonevu wakati akiomba ridhaa ya kupeperusha Bendera ya CCM.
Mtandao huu utakujulisha kitakachojiri katika mkutano huo.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago