François Hollande barani Afrika: hatua ya kwanza Benin

Rais wa Benin, Thomas Boni Yayi alikuwa alitembelea Ufaransa tarehe 9 Juni mwaka 2015, ambapo alipokelewa na François Hollande.
AFP PHOTO / POOL / THIBAULT CAMUS
Na RFI

Ni ziara ya kwanza ya François Hollande nchini Benin. Rais wa Ufaransa anatazamiwa kuwasili leo Jumatano usiku wa manane katika mji mkuu wa Benin, Cotonou, na anapania kutoa hotuba Alhamisi wiki hii. Hotuba ambayo itakua kama ujumbe wa kisiasa.

Benin, ni nchi ambayo viongozi hupishana madarakani - ni kwa mara ya tatu zoezi hili la kupishana madarakani linafanyika kwa kipindi cha miaka 25. Na hii ni nchi ambayo viongozi hawabadili Katiba ili wasaliye madarakani. Rais Boni Yayi ameahidi kwamba huenda akaondoka madarakani mwezi Aprili ujao.

Kwa hiyo ni nchini Benin ambapo François Hollande atatoa hotuba siku ya Alhamisi asubuhi wiki hii juu ya demokrasia. Hotuba ambayo itakua ya kipekee katika ziara yake barani Afrika, ambapo pia anatazamia kuendelea na ziara yake nchini Angola na Cameroon.

Demokrasia ni suala ambalo limekua likizuaa migogoro na mfarakano barani Afrika, wakati ambapo viongozi kadhaa wa Afrika wamekua wakijaribu kubadili katiba za nchi zao ili wasaliye madarakani. Hali hiyo imekua ikishuhudiwa nchini Burundi, Rwanda, Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo baadhi ya marais wa nchi hizo wanatazamia kubadidli Katiba ili wasaliye madarakani, na wengine walishindwa kubadili Katiba, lakini nia yao ni kusalia madarakani. Alhamisi asubuhi wiki hii, kama rais wa Ufaransa atatangaza wazi dhidi ya marekebisho ya Katiba, atapongezwa na wakaazi wa mji wa Cotonou.

■ Ziara hii nchini Benin inaashiria nini?

Ziara hii ni hatua zaidi katika mazungumzo ya kisiasa yaliyoanza muda mrefu uliopita. Rais Boni Yayi alimwalika François Hollande mwaka 2012 wakati ambapo alikuwa rais wa kwanza wa taifa hilo la kusini mwa Sahara kutembelea Ikulu ya Elysee. Kwa upande wake, rais wa Ufaransa alikuwa ameahidi kufanya ziara nchini Benin.

Ziara hii ni ishara ya kutambuliwa kwa Benin ambayo imejitolea kwa usalama wa kikanda barani Afrika. Wakati alipokua mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Boni Yayi aliunga mkono Ufaransa kuingilia kijeshi nchi ya Mali. Hata hivyo suala la Boko Haram litajadiliwa. Benin imeandaa kikosi cha wanajeshi 700 ambao bado wanasubiri kujiunga na wanajeshi wengine kutoka mataifa jirani kwa kupambana dhidi ya kundi hili la kigaidi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company