Obama |
Akizungumza katika mkutano na wanahabari ,Barrack Obama amesema kuwa amefanya mazungumzo ya kufana na waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na kwamba taifa hilo litakuwa thabiti wakati sauti zote zitakaposikika.
Bwana Desalegn amesema kuwa taifa hilo liko katika harakati ya kuweka demokrasia.
Vilevile Obama aliunga mkono maendeleo yalioafikiwa na Ethiopia kiuchumi pamoja na usalama wa kieneo.