Ukweli ni mzuri hata kama huupendi ama hauendani na Fikra zako,hakika CHADEMA imefanya kosa la kiuaminifu na kujipatia faida ya ushabiki na umati wa watu.
Na hasara kwamba imepoteza Imani yake kiuaminifu ambayo ilikuwa miongoni mwa wanachama na watu wenye mapenzi mema na Cha hicho.
Hotuba ya Mbowe ya jana kwa mtu aliye makini alitambua fika kwamba Lowasa amepokelewa CHADEMA sio kwamba anawezo mkubwa ama ametakasika kikashifa ila kwa sababu ni mtu mwenye watu wengi na sifa ama azima yao kubwa kama CHADEMA ni kupata watu wengi.
Kauli kama hii ukiitafakari kifilosofia unapata mantiki nzuri sana,ninayo mengi sana ya kuongea ila kwa leo sitakuchosha kwani makala ninyoianda haijakamilika ila ukweli ni kwamba CHADEMA imepoteza wanachama wazalendo na kujizolea mashabiki ambao ukweli ni kwamba wanafwata upepo tuu.
Nawamepoteza wazalendo wakindaki ndaki ambao mara zote walikuwa wepesi kuamini kilichokuwa kikisemwa na chama hicho juu ya CCM na Mafisadi,
Kwa mtaji huu ukweli ni kwamba watuhumiwa wote wa Ufisadi CCM wakihitaji kuja CHADEMA watapewa nafasi.
Madhara ya ushamba huu kisiasa hayawezi kujitokeza leo ila wakati na wasaa waja ndipo niyasemayo yatakuwa adhairi.