" Hakuna mtu anapaswa kuwa rais wa milele ", amesema Rais Obama katika hotuba yake kwa Umoja wa Afrika, akiwakemea viongozi wa Afrika wenye nia ya kusalia madarakani wakati muda wao wa kuondoka madarakani unapofika mwisho.
Na RFI
Rais wa Marekani Barrack Obama ametamatisha ziara yake barani Afrika, kwa ujumbe kwa viongozi wa bara hilo kuondoka madarakani muda wao unapofika mwisho.
Akizungumza katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa Jumanne wiki hii, Obama amewaambia viongozi wa Afrika kuwa tabia ya kukataa kuondoka madarakani inarudisha nyuma maendeleo ya demokrasia.
Ujumbe wa Obama ulimlenga rais wa Burundi Piere Nkurunziza ambaye alikataa kuondoka madarakani pamoja na viongozi wengine wanaobadilisha katiba ili kuendelea kusalia madarakani.(P.T)
Lambert Mende, msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ametupilia mbali kauli za viongozi wa nchi za kigeni.
" Rais Obama amerejelea maneno tunayosikia tangu miezi kadhaa kutoka kwa viongozi kadhaa wa Magharibi ambao, wakati wanatembelea Afrika, hawawezi kujizuia kutoa mafunzo kwa nchi za Afrika kama vile Afrika imekua nchi moja, ikiwa na tatizo moja na ufumbuzi mmoja, kana kwamba Afrika imekua na utaratibu wa Marekani kuhusu muda wa marais madarakani. Lakini sisi katika DRC tunahisi kuwa jambo hilo halituhusu, ingawa tunaona kuwa ni muhimu kuja na kutuambia jinsi ya kutatua matatizo yetu ya kitaasisi ... ", amesema Lambert Membe.
Waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, amekaribisha hotuba ya rais Barack Obama juu ya haja ya kuimarisha demokrasia barani Afrika. Waziri Mkuu wa Ethiopia, hata hivyo, alionekana akikosolewa na Barack Obama kwa kuwanyanyasa na kuwazuia jela waandishi wa habari pamoja na kuwa kandamiza wapinzani.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago