MBUNGE anayemaliza muda wake, Salvatory Machemli, amekuwa Mbunge wa kwanza wa jimbo kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kubwagwa kwenye kura za maoni zinazoendelea ndani ya chama hicho.
Machemli, aliyekuwa Mbunge wa Ukerewe mkoani Mwanza, alijikuta akishindwa kupata kura za kutosha katika uchaguzi huo uliofanyika juzi mjini Nansio, Ukerewe.
Awali, uongozi wa Chadema Makao Makuu ulikuwa na mapendekezo kwamba wabunge wa majimbo wa chama hicho wapite bila kupingwa na ingawa wengi walikuwa na wapinzani, wamefanikiwa kuvuka kizingizi cha kura za maoni isipokuwa Machemli.
Aliyembwaga Machemli ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Joseph Mkundi, aliyepata kura 232 kati ya 466 zilizopigwa, akiwashinda wagombea wengine tisa huku Machemli akiambulia kura 74.
Hata kabla ya matokeo kutangazwa, tayari Machemli aliondoka ukumbini na taarifa ambazo hazikuthibitishwa jana zinasema kwamba jana alikuwa ‘akiendesha operesheni’ maalumu ya kuwanyang’anya pikipiki wapambe wake kadhaa aliowapa wamsaidie kufanya kampeni.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago