Rais wa Uganda, Kaguta Yoweri Museveni, ameteuliwa kuwa msuluhishi mpya katika mgogoro wa Burundi.
Reuters/James Akena
Na RFI
Viongozi wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki wamemteua Jumatatu wiki hii katika mkutano wao jijini Dar es Salaam, rais wa Uganda, Kaguta Yoweri Museveni, kuwa msuluhishi mpya wa mgogoro unaoendelea nchini Burundi.
Mgogoro huo ulizuka wakati rais Pierre Nkurunziza alitangaza kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais.
Hata hivyo rais wa Burundi Pierre Nkurunziza hakushiriki mkutano huo wa marais. Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashiriki wameitaka kwa mara nyingine tena serikali ya Burundi kuahirisha uchaguzi wa urais hadi Julai 30. Hata hivyo uchaguzi wa urais nchini Burundi umepangwa kufanyika tarehe 15 Juni mwaka huu.
" Pendekezo hilo la kuahirisha uchaguzi kwa kipindi chote hicho ni kutaka kumpa muda msuluhishi huyo mpya kuongoza mazungumzo ”, amesema katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera, baada tu ya mkutano wa marais wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kumalizika.
Taarifa ambayo haijathibitishwa inaarifu kwamba huenda msuluhishi wa Umoja wa Mataifa Abdoulaye Bathily amejiuzulu kwenye nafasi hiyo.
Haijafahamika iwapo serikali ya Burundi itakubali kuahirisha uchaguzi wa urais, kwani hata awali Umoja wa Afrika uliiomba serikali ya Burundi kuahirisha uchaguzi wa wabunge na madiwani na ule wa urais, lakini uchaguzi wa wabunge namadiwani ulifanyika Juni 29, na uchaguzi wa urais unatazamiwa kufanyika Julai 15.
Hata hivyo upinzani umetupilia mbali mapendekezo ya marais wa Jumuiya ya Afrika MAshariki, ambao hawakuzungumzia chanzo cha mgogoro wa Burundi ikiwa ni pamoja na rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula watatu. Jean Minani, mmoja kati ya viongozi wa upinzani ambaye alijielekeza jijini Dar es Salaam, amesema Jumuiya ya Afrika Mashariki haina utashi wa kutatua mgogoro wa Burundi, bali inampa nafasi Nkurunziza kuendelea kuwania muhula wa tatu. Jean Minani amesema msimamo wao bado ni ule ule : kumshinikiza Pierre Nkurunziza kutowania muhula wa tatu, kwani ni kinyume na Katiba ya nchi na Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago