Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano ofisini kwake jijini Dar es Salaam, kuhusiana na wahamiaji haramu wanayo jiandikisha katika Daftari la wapiga kura katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Raia wa kigeni ambao wamejaribu kujipatia vitambulisho vya kupigia kura wamefikia 2,040.
Hayo yamesemwa na Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano ofisini kwao jijini Dar es Salaam leo.
Imeelezwa kuwa Kagera walikamatwa watu 708, Mara 619, Tanga 348,Kigoma 254, Rukwa 13, Kilimanjaro 12, Ruvuma 9, Geita 6, Shinyanga 7, Mtwara 3, Pwani 2, Mbeya 1, Morogoro 1 na Dar es Salaam 65.
Katika hatua nyingine, Irovya amesema kuwa wananchi waliochukua pasi za kusafiria, zinapoisha muda wake ni lazima wazibadilishe na kupewa nyingine wakati wowote wanapozihitaji. Amesema kuwa wananchi wanapaswa kwenda katika ofisi za uhamiaji ili kupata pasi mpya na siyo mahali kwingine. [via Michuzi blog]
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago