Picha hii imepigwa kupitia video iliyorushwa kwenye runinga ya WHSV-TV katika mji wa Harrisonburg, Virginia, inaonyesha Vester Lee Flanagan, mtu anayetuhumiwa kuwaua kwa kuwapiga risasi mwandishi wa habari na mpiga picha kituo cha TV wakati wa mahojiano ya
AFP/WHSV TV/AFP
Na RFI
Mtu ambaye aliyewaua kwa risasi waandishi wa habari wawili wa kituo cha runinga cha WDBJ7 katika jimbo la Virginia Jumatano wiki hii, nchini Marekani, amefariki kufuatia jeraha alilopata, baada ya kujipiga risasi, viongozi wa jimbo la Virginia wamethibitisha.
" Mtuhumiwa katika mauaji hao amefariki akiwa katika hospitali ya Fairfax Inova, kaskazini mwa Virginia ", amesema mkuu wa Kaunti ya (mashariki), Bill Overton, katika mkutano na waandishi wa habari.
Vester Lee Flanagan II, ambaye pia amekua akijiita Bryce Williams, alitimka mara baada ya kuwapiga risasi waandishi wa habari wawili ambao walikuwa wakifanya mahojiano ya moja kwa moja ya runinga na kiongozi wa shirikisho la wafanyabiashara wa kijiji kidgo cha Virginia(mashariki) muda mfupi kabla ya 1:00, kwa mujibu wa polisi.
Akiwa mafichoni tangu Jumatano asubuhi wiki hii, mtu huyo mwenye umri wa miaka 41, hatimaye afisa wa polisi alimuona akiendesha gari. " Alikataa kusimama na kuendelea kwa kasi ", amesema Rick Garletz, afisa wa polisi katika jimbo la Virginia, wakati wamkutano huo na waandishi wa habari.
Mwandishi wa habari mwenye umri wa miaka 24 na mpiga picha mwenye umri wa miaka 27 wa kituo cha WDBJ7 katika jimbo la Virginia, mashariki mwa Marekani wameuawa kwa kupigwa risasi Jumatano Agosti 26.
Mwandishi wa habari wa kike na mpiga picha wa kituo cha WDBJ7-TV katika jimbo la Virginia wameuawa Jumatano asubuhi wiki hii wakati wa matangazo ya moja kwa moja kutoka Kaunti ya Bedford (mashariki mwa Marekani). " Tumepata taarifa kwa msaada wa polisi na wafanyakazi wetu wenyewe kwamba Alison na Adamu wamefariki asubuhi hii muda mfupi baada ya 12:45 wakati risasi zilisikika ", amesema Jeffrey Marks, mkurugenzi mkuu wa WDBJ7, kwenye runinga ya CNN .
Kituo kilichoajiri waandishi hao cha WDBJ7 kimesema mwandishi huyo wa habari Alison Parker na mpiga picha Adam Ward walikufa katika tukio hilo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa la AFP, picha ziliyopigwa na mpiga picha wa WDBJ7-TV kabla ya kuuawa, zinaonyesha miguu ya mshambuliaji akimpiga risasi mwandishi wa habari wa kike, huku kelele ikisikika. Video hii itakuwa muhimu sana kwa polisi, ambayo imekua ikimsaka kwa udi na uvumba mapema Jumatano asubuhi mru aliyehusika na shambulio hilo.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago