MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Abdallah Bulembo amepiga marufuku uwanja wa jumuiya hiyo uliopo eneo la Milango Kumi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kutumika kwa mikutano ya kampeni za siasa kwa vyama vinavyounda umoja wa Ukawa kwani uwanja huo ni rasilimali ya wanaCCM.
Bulembo alitoa onyo hilo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati alipomkaribisha Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli aliyefika kwa wakazi wa Mji wa Kahama kwa lengo la kuomba kura.
Alimtaka Dk Magufuli autumie uwanja huo vyema kuomba kura kwani ni wake kwa kuwa baadaye ndiye atakayekuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa pindi atakapochaguliwa.
Alimweleza mgombea urais mbele ya wananchi kuwa uwanja huo ni mali ya wanaCCM kupitia Wazazi ambao ndio wamiliki na wameuweka mahususi kwa kuandaa mikakati ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi katika eneo hilo, hivyo uwanja huo usitumike kwa siasa na vyama pinzani badala yake CCM pekee wataendelea kuutumia.
“Mambo yakiwa mazuri hapa tulipo watajenga shule ya ufundi ‘Veta,’ uwanja huu Chadema hawaruhusiwi kufanya mikutano ya kampeni za siasa ya Ukawa hapa, siyo eneo lao, tusiwaone hapa watafanya mikutano ya kampeni za CCM pekee.”
Pia Bulembo aliwaeleza wananchi hao kuwa Ukawa kuongoza nchi ni ndoto kwani Mgombea urais kwa tiketi ya CCM amefanikisha kupiga mikutano mingi huku akisema mikutano rasmi kwa siku moja ni 110 isiyo kuwa rasmi ni 420, na kutembea umbali wa kilometa 15,600 kwa siku kitu ambacho wao hawana uwezo nacho.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago