Image captionWaandamanaji nje ya makao makuu ya rais nchini Burkina Faso
Rais wa mpito Michel Kafando amepokonywa madaraka yake huku serikali yake ikivunjiliwa mbali, kwa mujibu wa afisa mmoja wa jeshi aliyezungumza katika runinga ya taifa nchini humo RTB.
''Tumeweka baraza la kitaifa la demokrasia litakalopanga uchaguzi wa kidemokrasia,'' alisema afisa huyo aliyevaa sare za kijeshi ambaye hakutambulika.
Hatua hiyo inajiri baada ya viongozi wa serikali hiyo ya mpito nchini Burkina Faso kuzuiliwa na walinzi wanaomtii aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Blaise Campaore aliyeng'atuliwa mamlakani.Image captionAfisa aliyetangaza kuvunjwa kwa serikali Burkina faso
Rais Michel Kafando na waziri mkuu Isaac Zida walizuiliwa katika mkutano wa mawaziri katika makao ya rais katika mji mkuu wa Ougadougou.
Hatua hiyo inajiri siku mbili baada ya tume kutoa agizo la kuvunjiliwa mbali kwa kikosi cha walinzi wa rais RSP.
Risasi zilipigwa ili kuwatawanya waandamanji waliopiga kambi nje ya makao hayo ambapo wanaozuiliwa bado wapo.Image captionRais wa Mpito Michel Kafando na waziri mkuu Isaac Zida
Hakuna majeraha yalioripotiwa lakini kumedaiwa kuwepo kwa hali ya wasiwasi huku maduka yakifunga biashara mapema na raia wengi kuelekea majumbani mwao.
Maandamano ya ghasia yalioshirikisha kulichoma bunge yalimshinikiza rais aliyehudumu kwa mda mrefu Campaore kung'atuka mamlakani mnamo mwezi Octoba mwaka 2014.
Bwana kafando na luteni kanali Zida walipewa jukumu la kuandaa uchaguzi mpya wa urais mwezi ujao.
Wao pamoja na maafisa wengine walitekwa nyara na walinzi wa RSP, mkuu wa bunge la mpito Moumina Cherrif Sy,alisema katika taarifa.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago