Manowari hiyo ina uwezo wa kubeba ndege 40
Ufaransa imesema itatuma manowari yake kubwa zaidi ya kivita kusaidia katika operesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji wa Islamic State (IS) nchini Syria na Iraq.
Kutumiwa kwa meli hiyo ya kivita kutasaidia kupunguza muda unaotumiwa na ndege za kivita kutekeleza mashambulio ya kutoka angani.
Ufaransa imekuwa ikishambulia IS chini ya muungano unaoongozwa na Marekani tangu Septemba 2014.
Septemba mwaka huu, Ufaransa ilianza kutekeleza mashambulio ya kijeshi ya kutoka angani dhidi ya IS.
Manowari hiyo ya kubeba ndege kwa jina Charles de Gaulle tayari imetumiwa awali kukabiliana na wapiganaji hao wa Kiislamu.
Meli hiyo, ambayo ndiyo pekee ya aina yake kumilikiwa na Ufaransa, ilitumiwa kama kituo cha kutua na kupaa kwa ndege za kijeshi za Ufaransa eneo la Ghuba kuanzia Februari hadi Aprili.
Ufaransa kwa sasa inatumia ndege sita aina ya Mirage ambazo zinahudumu kutoka Jordan na ndege sita aina ya Rafale ambazo hushambulia IS kutoka Muungano wa Milki za Kiarabu.Image copyrightAFP
Manowari hiyo ina uwezo wa kubeba ndege 40 kwa siku na kufanikisha safari 100 za ndege kila sku.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema uamuzi huo ni mwafaka na utasaidia Ufaransa kusaidiana vyema na washirika wake.
Serikali ya Ufaransa imesema mashambulio dhidi ya IS ni hatua ya kujikinga, baada ya wanamgambo wa IS kuua watu 17 katika mashambulio mawili mjini Paris mapema mwaka huu.
Tangu wakati huo, ndege za kijeshi zimeshambulia ngome za IS mara 271, kwa mujibu wa shirika la habari za AFP. CHANZO BBC SWAHILI
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago