DAR YA ZINDUKA KWA USAFI

Mh. Silaa,Mh. Mushi na Mh. Chiligati washirikiana na Kampuni ya Green WastePro kufanya usafi katika fukwe ya Ocean Road jijini Dar leo

Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mh. Raymond Mushi (katikati),Meya wa Manispaa ya Ilala,Mstahiki Jerry Silaa na Mh. John Chiligati wakishirikiana kwa pamoja kufanya usafi katika Fukwe ya Ocean Road jijini Dar es Salaam,mapema leo asubuhi ikiwa ni Muendelezo wa kuhakikisha Halmashauri ya Ilala inaongoza kwa Usafi jijini Dar.Zoezi hilo limeendeshwa na Kampuni ya Kisasa ya Green WastePro Ltd ambayo ndio yenye Zabuni ya kufanya Usafi katika maeneo mbali mbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilala.na leo wameanza na Fukwe hii na kisha baadae wanaenda kwenye Fukwe ya Mchafu koge na sehemu nyingine nyingi.
Add caption

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya kisasa ya Usafi ya Green WastePro Ltd,Anthony Mark Shayo (kushoto) akishirikiana na Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni yake hiyo kuondoa tairi chakavu lililokuwa limejifukia kwenye mchanga wa ufukwe wa Ocean Road jijini Dar,wakati wa zoezi la kufanya usafi katika Ufukwe huo lililoanza kufanyika mapema leo asubuhi na kuudhuliwa na watu mbali mbali.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya kisasa ya Usafi ya Green WastePro Ltd wakiendelea na zoezi la kufanya usafi katika eneo la fukwe ya Ocean Road jijini Dar mapema leo asubuhi.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya kisasa ya Usafi ya Green WastePro Ltd,Anthony Mark Shayo akiendelea kuwajibika kwenye zoezi hilo ambalo linaendelea hadi hivi sasa kwenye fukwe ya Ocean Road,jijini Dar.
Baadhi ya wadau wa Kigeni waliojitokeza kufanyikisha zoezi hilo nao wakiendelea kuwajibika.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mh. Raymond Mushi (wa pili kushoto) akimuonyesha kitu Meya wa Manispaa ya Ilala,Mstahiki Jerry Silaa (wa tatu kushoto) wakati wa zoezi la kufanya usafi katika Ufukwe wa Ocean Road jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi.Zoezi hilo limeendeshwa na Kampuni ya Kisasa ya Green WastePro Ltd ambayo ndio yenye Zabuni ya kufanya Usafi katika maeneo mbali mbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilala.Kushoto ni Mh. John Chiligati ambaye nae alishiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
Waheshimiwa wakikusanya taka.
Waheshimiwa wakiendelea na usahi katika ufukwe wa Ocean Road jijini Dar mapema leo asubuhi.
Baadhi ya vijana wa Ilala Jogging Club wakishiriki kwenye zoezi la kufanya usafi kwenye Zoezi la kufanya usafi katika Ufukwe wa Ocean Road lililoendeshwa na Kampuni ya Kisasa ya Green WastePro Ltd ambayo ndio yenye Zabuni ya kufanya Usafi katika maeneo mbali mbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilala.
Zoezi likiendelea.
 Meya wa Manispaa ya Ilala,Mstahiki Jerry Silaa (katikati waliosimama) akizungumza na Baadhi ya vijana wa Ilala Jogging Club walioamua kuacha mazoezi waliyokuwa wakiyafanya kwenye Ufukwe huo wa Ocean Road na kuamua kusaidia kufanya usafi kwenye ufukwe huo mapema leo asubuhi.Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mh. Raymond Mushi.
 Baadi ya wafanyakazi wa Kampuni ya kisasa ya Usafi ya Green WastePro Ltd wakikusanya sehemu ya takataka zilizotokewa kwenye Ufukwe huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mh. Raymond Mushi (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Meya wa Manispaa ya Ilala,Mstahiki Jerry Silaa wakati wa zoezi la kufanya usafi katika Ufukwe wa Ocean Road jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi.
Jamaa nao walipata tenda ya kunoa Makwanja yoye ya kufyekea majani yaliyokuwepo hapo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company