KUPIIA JASHO AMBALO HUONESHA HASIRA
Wenyewe hawajui lakini, mwamke anaweza kunusa hasira, naam ikiwe mumewe ana hasira hata akikaa kimya , mkewe atakuwa wakwanza kujua kwamba mmmh! leo kumeharibika.
Mwanamke pia anaweza kunusa uogoa wa mumewe.
Dr Gün Semin wa Utrecht University, Ujerumani anasema hii ni kutokana na jasho la mwanamume!
Utafiti unaonyesha kuwa jasho analotoka mwanamume linatuma ujumbe katika kiwili wili cha mwanamke na kumuambukiza hali unayosikia bila ya wewe kumuambia kitu.. Jasho lako linatuma ujumbe kwa mkeo au kwa mchumba wako.
Ukiwa wewe mwanamume umeshutshwa na kitu au umebabaika au umeogopa au ana hasira. Jasho lako litasema. Na System ya mama itapokea ujumbe!
Dr Gün Semin wa Ujerumani anasema mwanamume akikasiria anatoa jasho lenye kemikali aina fulani. Akiwa na uoga anatokwa na jasho aina tofauti.
Ndio maana mkeo au mchumba wako atakuuliza kuna nini lakini? Hata ukikataa mwili wake unamuashiria kwamba lazima kuna kitu. Sio ati wao ni wajanja sana lakini jasho lako limetoa chembechembe fulani kulinagani na hali yao na hivyo kutuma ujumbe wa siri kwa system ya mama.
Ni majaliwa ya wanawake hayo.
....
Wanasayasi wanasema kipepeo ana uwezo wa kunusu kipepeo mchumba wake au anayemfaa hata akiwa maili 7 au nani hivi.
Kipepeo atanusa nakujua kiboko yangu anakuja japo yuko kilomita nyingi.
Nani mwenye uwezo mkubwa zaidi wa kunusa? Kwa wanyama ni Dubu, yaani bear, sio teddy bear.
Baharini ni papa. Papa anaweza kunusa hata damu amboyo bado ingali ndani ya samaki mwengine. Ni papa huyo.
..............
Wanasayansi wanasema kuwa wanawake ni viumbe wa ajabu!
Katika mahusiano ya kawaida, urafiki tu wa kimapenzi, boy friend na girl friend wanawake bila ya wao kujua huvutiwa na watu wakaidi, watukutu watu wenye miguvu kuvu, misuli misulu, watu wenye vimo virefu kwa kiingereza hao wabajulikana kama Alfa men.
wabasayansi wanasema watu wenye vurugu vurugu , watundu wanauwezo mkubwa wa kutongoza.
Pengine hii nikutokana na sababu ya kutoogopa kukataliwa.
........
Lakini katika ndoa wanawake bila ya wao hata kujijua huvutiwa na watu wadhaifu , watu waungwana, wastaarabu, wenye hekima watu wenye vimo vya wastani.
......
Watafiti wa maswala ya kijamii na mahusiano wanasema kuwa kwa akina dada wengi katika ndoa huvutiwa na watu wasio na misuli, wenye vimo vya wastani au hata wafupi - hawa kimombo wanajulikana kama Beta men- B-E-T-A, Beta, baada ya Alfa , kuna Beta katika alphabeti za kirumi.
Kwanini ieve hivyo.
Sayanmsi ya mahusiana inasema kuwa watu wasiokuwa nguvu, vimo vya kutisha au misulu eti, eti wanajali sana familkia zao na wake zao.
Maelezo ni kwamba
kwa kuwa hawaezi kushndana katika ulimwerngu wa mahaba kwa kutumia nguvu na kifua basi mwenyezi mungu amewapa sifa za kuwa wakarimu, wenye kutoa, kujali wapenzi wao , na kama njia ya kutinza ndo zao Mungu amewapa watu sampuli hiyo uwezo wa kuwa waaminifu. Wasipo kuwa hivyo kuna hofu ya kutorokwa!
Ni sayansi ya mahusiano!
.........
Jee unajua kuwa kufanya kazi usiku ni hatari kwa akina mama? Na inaweza kusababisha kifo?
Utafiti uliofanywa na madaktari nchini Uingereza umegundua kuwa wanawake wanaopendelea kufanya kazi usiku wanahatari ya kupatikana na sartani ya matiti- breast cancer.
Katika kichwa cha Kazi za usiku zinasababisha vifo 500 kila mwaka nchini Uingereza utafiti hunasema shift za usiku ni hatari kwa akina amma.
Dr Lesley Rushton, wa Imperial College Mjini London anasema Mawanamke akifanya kazi ya usiku kwa wastani ya siku tatu kwa wiki kwa miaka sita - anakaribisha kansa ya matiti.
Kufanya kazi usiku au kukosa usingizi kwa akina mama kunatatiza utengenezaji wa homoni ya ya MELATONI, hii ni chembechembe inayosaidia usingizi na hii inasadikiwa kuwa na uwezo wa zuia kansa.
................
Wanasayansi wana mambo!
Dawa hii iliyovumbuliwa Ujerumani inaitwa FIDELITY HORMON. Dawa ya uaminifu! Au kampuni hiyo ya ujereumani imeipa dawa hiyo jina la CUDDLE DRUG! Dawa ya kukumbatiana.
Dr René Hurlemann, of Bonn University nchini Ujerumani anasema mwanamume akipewa dawa hii ya kumeza huyeyuka na kuingia katika damu, hivyo mwanamke mrembo akipita karibu, basi mume analazimika kukaa umbali wa inchi sita . Mume bila kujua damu yake itakuwa haipatani na mwanamke mwengine mbali na mkewe.
Mwanamke huyo akiwa mrembo zaidi , ndio dawa inafanya kazi vizuri zaidi. Ni FIDELITY HORMON. Tembe za uaminifu.
.....
Ipada inaweza kupiga picha ya video, picha ya kawaida , kucheza muziki , kuzuru mtandao na mambo mewngi tu.
Lakini ujajua kwamba ukiwa na tabia ya kutumia Ipad usiku usiku huenda ukapatikana na matatizo ya moyo au msongo au kudorora kwa afya, yaani depression?
Utafiti pia unasema kuwa ukiwa na tabia ya kuangali televisheni hadi usiku mpevu kila mara basi unakaribisha maradhi ya moyo au depression.-kudorora kwa afya.
Profesa Samer Hattar anasema wa Marekani anasema utafiti umegundua kuwa televisheni na komputa ya iPad inatoa mwanga usistahili wakati mwili unahitajika kulala.
Hivyo kutumia iPad na televisheni usiku sana inaweza kusababisha maradhi ya moyo au mtu kukosa raha maishani au kutompenda starehe au mkuwa mtu pweke, kutumia iPad au televsiheni kila mara usiku sana kunasababisha upweke.
Hi