Hospitali ya Taifa ya Muhimbili nchini Tanzania imeanzisha wodi maalumu inayotoa huduma mpya, maarufu kama Kangaroo ya kuwatunza watoto wanaozaliwa kabla ya siku zao bila ya kutumia mashine za inkubeta.
Huduma hiyo hutumika kwa mama kufungiwa mtoto kwa kitambaa maalumu kwenye tumbo lake, mfano wa mnyama Kangaroo anavyombeba mtoto wake, lengo ikiwa ni kumsaidia mtoto kupata joto na kumfanya awe karibu na mamake tofauti na inavyokuwa katika mashine ili aweze kukuwab haraka.Mwandishi wetu Aboubakar Famau kutoka Dar es Salaam ametuandalia taarifa ifuatayo