ECOWAS yaomba isaidiwe Mali

Viongozi wa nchi za Afrika magharibi wameomba msaada wa kimataifa kugharimia majeshi yao kuingilia kati nchini Mali.

Wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali
Walisema hayo kwenye mkutano unaofanywa Abidjan, Ivory Coast.
Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, ambaye amehudhuria mkutano huo, ameshikilia kuwa majeshi ya Afrika yatashika uongozi wa operesheni za kijeshi nchini Mali katika majuma yajayo.
Nchi kadha za Afrika Magharibi zimeahidi kujitolea kwa wanajeshi ili kulisaidia jeshi la Ufaransa katika mapambano yake dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu, lakini nchi hizo zina shida za usafiri na fedha na hivo zinaweza kuchelewa kutuma wanajeshi wao Mali.
Hata hivo, Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, amesisitiza kuwa majeshi ya Afrika yatachukua nafasi ya Ufaransa katika majuma tu yajayo.
Lakini uwezo mdogo wa wanajeshi wa Afrika Magharibi kushiriki kwenye vita kaskazini mwa Mali huenda ukaifanya Ufaransa ilazimike kubaki vitani kwa miezi kadha ijayo.
Wanabalozi wa mataifa ya magharibi wanasema kuwa kisa cha wageni kutekwa nchini Algeria, kimeyafanya mataifa makuu kuamini kuwa lazima yapambane na makundi ya wapiganaji wa Kiislamu yalioko kaskazini mwa Mal
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company