Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili nyumbani kwa Balozi Hongera Witson Muyola wa shina namba 8 Tawi la Mtunduru ambapo alifanya mazungumzo na Balozi huyo ambaye ndio msingi mkubwa wa wanachama .
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akipanda mti kwenye eneo linalojengwa zahanati wa kata ya Isansa,wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa Mbozi Ndugu Geofrey Zambi akihutubia wakazi wa Vwawa na kusema kuna matumizi mabaya ya pesa katika halmashauri za mkoa wa Mbeya na kusababisha kukwama kwa shughuli nyingi za maendeleo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Vwawa wilayani Mbozi ambapo aliwaambia CCM hii ni CCM inayofanya kazi na asiyeweza kufanya kazi na CCM hii awapishe,kwani wapo kwa ajili ya kutetea wakulima na wafanyakazi na si vinginevyo alisisitiza Vijana kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwani ndio njia nzuri ya kuleta maendeleo na si kuami kuwa Katiba mpya inaweza badilisha maisha yao.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago