Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amemshukuru Rais Xi Jinping wa China kwa uungaji mkono wake kwa mradi wa ujenzi wa reli, na kusema hii ni ishara kuwa yeye ni rafiki wa kweli wa Kenya. Rais Kenyatta alisema hayo wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa reli hiyo mjini Mombasa.
Akiongea katika hafla hiyo Balozi wa China nchini Kenya Bw Liu Guangyuan amesema ujenzi wa reli ni chaguo la kimkakati kwa Kenya na reli zimetoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya uchumi wa China katika miaka 30 iliyopita.
Naibu Rais wa Kenya Bw William Ruto amesema uzinduzi wa ujenzi wa reli hiyo ni hatua muhimu ya utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na muungano wa Jubilee wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu.