Sehemu ya wapiganaji toka makundi ya waasi yanayofanya shughuli zao mashariki mwa DRC
Reuters
Na
Sabina Chrispine NabigamboWanamgambo wanaoshutumiwa kwa ubakaji na mauaji ya raia katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesema wako tayari kuweka silaha zao chini, mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa amesema jana Ijumaa, na kulitaka jeshi nchini humo kurejesha utulivu katika maeneo ya jirani.
Wanamgambo wa kujilinda wakiongozwa na jenerali Sheka Ntabo Ntaberi anayejulikana kama Sheka Mai Mai limekuwepo nchini humo kwa miaka mitatu sasa, likipambana na majeshi pinzani kwa ajili ya udhibiti wa migodi ya dhahabu.
Mwishoni mwa mwezi Oktoba, Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO,kiliarifu kwamba takribani raia 34, ikiwa ni pamoja na watoto 20 wenye umri kati ya miezi sita na miaka 17 waliuawa kwa ghasia kubwana na kundi la Sheka Mai Mai katika vijiji vya jimbo la Masisi huko Kivu Kaskazini.