Ndege ya polisi nchini Scottland yaanguka na kusababisha madhara makubwa na uwezekano wa vifo


Muonekano wa eneo ilikotokea ajali ya ndege ya polisi mjini Glasgow nchini Scottland
heraldscotland.com
Na Sabina Chrispine Nabigambo

Helikopta ya polisi imeanguka juu ya paa la mgahawa mmoja kwenye mji wenye msongamano katika mji wa Glasgow nchini Scottland na kusababisha madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja uwezekano wa vifo na kuacha watu kadhaa wamenaswa katika kifusi, maafisa wamesema leo Jumamosi
Kikosi cha Huduma za dharura kimesema kuwa wamekuwa wakiwasiliana na idadi isiyojulikana ya watu ndani ya mabaki ya mgahawa wa Clutha , ambapo zaidi ya walevi 100 walikuwa wakisikiliza bendi kabla ya tukio la ajali Ijumaa usiku

Waziri wa Kwanza wa Scottland Alex Salmond amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa Kutokana na tukio la kiwango hicho ni lazima wote kujiandaa kwa ajili ya uwezekano wa taarifa za vifo.

Polisi wanasema kulikuwa na maafisa wawili wa polisi na marubani wawili raia wa kawaida ndani ya ndege hiyo ya Eurocopter EC135 lakini hakutoa maelezo zaidi kuhusu hali zao, na kusema kuwa ilikuwa ni mapema mno kusema chanzo kilichosababisha ajali hiyo.
www.hakileo.blogspot.com
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company