Mkuu wa shirika la kimataifa la IAEA asema itachukua muda kuthibitisha makubaliano ya Iran na mataifa yenye nguvu kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran


Mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za Atomic IAEA Yuyika Amano
REUTERS/Toru Hanai
Na Sabina Chrispine Nabigambo

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia nguvu za Atomiki IAEA leo Alhamisi ameonya kuwa itachukua muda katika kushughulikia jinsi ya kuthibitisha matakwa ya Iran na mataifa yenye nguvu katika makubaliano mapya ya kihistoria kuhusu mpango wake wa Nyuklia.
Mkuu huyo Yuyika Amano amesema kuwa kwa sasa wanaangalia njia ambayo kwayo ishara za makubaliano zenye uhusiano na shirika hilo zinaweza kutekelezwa.

Akizungumza kwenye mkutano wa ndani wa bodi ya magavana wa shirika hilo Amano ameongeza kuwa hiyo itajumuisha suala la ufadhili wa kifedha na wafanyakazi, uchambuzi ambao utachukua muda.

Mapema siku ya Jumapili Iran ilikubaliana na mataifa yenye nguvu duniani kama Marekani, China, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ambayo yalikuwa yakikutana mjini Geneva Uswisi kusitisha sehemu ya mpango wake wa nyuklia kwa muda wa miezi sita ili kurahisishiwa vikwazo.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company