Admeri Habibullah Sayyari Kamanda wa Jeshi la Majini la Iran
Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kikosi cha majini cha taifa hili kiko tayari kutetea na kulinda doria katika maji ya taifa hili hususan Ghuba ya Uajemi. Admeri Habibullah Sayyari amesisitiza kuwa, kikosi cha wanamajaji cha Iran kiko macho na kimejiandaa kikamilifu kukabiliana na chokochoko yoyote ile kutoka kwa adui. Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Iran kwa kutumia uwezo wa jeshi lake la wanamaji litazima njama zote za maadui katika eneo hili. Admeri Habibullah Sayyari ameongeza kuwa, vikosi hivyo viko tayari kukabiliana na harakati yoyote inayoweza kujitokeza ya maadui. Amesema, hii leo jeshi la majini la Iran ni miongoni mwa vikosi vya majini vyenye nguvu ulimwenguni kutokana na kutumia mbinu za kisasa kabisa tena kwa kutumia wataalamu na zana za kijeshi zilizotengenezwa hapa nchini.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago