Majeshi ya Ufaransa yakilinda uwanja wa ndege wa Bangui.
Ufaransa inaongeza wanajeshi 1,000 zaidi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kusaidia kikosi cha Umoja wa Afrika kinachojaribu kurejesha ushwari nchini humo.
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves-Le Drian alisema jana kuwa wanajeshi hao watahudumu nchini humo kwa miezi sita hivi. Kwa sasa Ufaransa ina wanajeshi 400 katika mji mkuu Bangui.
Kikosi hicho cha walinda amani kilichoko nchini humo ni 2,500, na inategemewa kitaongezwa kufikia 3,500. Umoja wa Afrika utachukua jukumu la tume hiyo ya walinda amani mwezi ujao, kulinda raia na kurejesha uthabiti wa serikali kuu.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago