Waziri wa usalama wa Israel akutana na msuluhishi wa Uingereza kwenye mazungumzo ya mpango wa Nyuklia wa Iran


Waziri wa mambo ya usalama wa Israel Yuval Steinitz
timesofisrael.com
Waziri wa mambo ya usalama wa Israel Yuval Steinitz amekutana na msuluhishi wa Uingereza kwenye mazungumzo ya mpango wa nyuklia wa Iran kama sehemu ya juhudi za kushawishi muonekano wa makubaliano ya mwisho ya mpango huo.Israeli imelaani mpenyo wa makubaliano yaliyofikiwa na mataifa yenye nguvu duniani na Iran mjini Geneva siku ya Jumapili ambapo Tehran imekubali kusitisha baadhi ya mipango yake ya Nyuklia ili kurahisisha vikwazo dhidi ya taifa hilo ambapo Israel inaona kuwa makubaliano hayo ni kosa la kihistoria.

Wakati wa mkutano mjini Yerusalem msuluhishi mkuu wa Uingereza Simon Gass na maafisa wa Israel wakiongozwa na Steinitz wamefikia makubaliano kuhusu tofauti zilizopo na kujadili kwa kina makubaliano hayo na mantiki yake.

Aidha majadiliano ya awali kuhusu sura ya makubaliano ya mwisho pia yalianza wakati wa mkutano huo ambapo licha ya kutkinzana kwa mwazo , mazungumzo yalifanyika katika mazingira ya wazi na ya urafiki.

Msemaji wa Steinitz amesema kuwa jana Jumanne Steinitz amekutana na mkuu wa msuluhishi mkuu wa Ufaransa Jacques Audibert mjini Yerusalem kujadili kuhusu makubaliano ya mpito na makubaliano ya mwisho.

Uingereza na Ufaransa , sambamba na Marekani, Urusi, China na Ujerumani kwa pamoja wanaunda mataifa yenye nguvu duniani ambayo yalijadili makubaliano hayo , ambayo wanasema ni hatua muhimu kuelekea kupunguza kuongezeka kwa vitisho vya kijeshi Mashariki ya Kati.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company