Mtoto akipimwa mzunguko wa mkono kufahamu iwapo na utapiamlo
Shirika la afya duniani, WHO leo limetoa mwongozo mpya wa tiba kwa watoto wenye unyafuzi au utapiamlo uliokithiri unaoripotiwa kuwa tatizo kubwa kwa watoto Milioni 20 duniani kote wenye umri wa chini ya miaka mitano. George Njogopa na ripoti kamili.
WHO inasema kuwa hali mbaya ya utapiamlo inajitokeza wakati ambapo mtoto anakuwa kwenye hali kushindwa ama kukosa kabisa kile kinachoitwa utoaji wa jasho na hivyo kuhatarisha afya yake
Hali hii inajitokeza kutokana na mwili wa mtoto kukosa virutubisho muhimu ikiwemo protini ambayo kimsingi inatokana na ukosefu wa chakula bora. Pia inachangiwa na mazingira mengine ya kiafya anayokumbana nayo mtoto katika maisha yake ya kila siku.
Tatizohilolinaweza kubainika katika wakati ambapo kumejitokeza mambo kadhaa ikiwemo sehemu ya juu ya mikono ya mtoto kupoteza uzito na wakati mwingine kusinyaa kwa kiwango cha milimita 115.
Dk Fransesco Branca ni Mkurugenzi wa kitengo cha Lishe kinachohusika na masuala ya afya na maendeleo.